Email: info@jkuz.go.tz  |  P.o.Box: 985  |  Tel: 0242238030  |  Fax: 0242232149


Logo
HABARI NA MATUKI0

WAHITIMU WA MAFUNZO YA HUDUMA YA MWANZO MKUPUO 01 WAKIMALIZA MAFUNZO YAO HAPO KATIKA HOSPITALI YA MAKAO MAKUU SAATENI

Created at 1 month ago

Mkuu wa JKUZ

Madaktari wa Hospitali ya Jeshi la Kujenga Uchumi(JKU) wametakiwa kuongeza bidii katika kuboresha huduma za Afya ili kuwasaidia wapiganaji na jamii kwa ujumla.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Wakala wa Ulinzi wa JKU Kanali Jabir Haji Hamza wakati alipokua akifunga Mafunzo ya Huduma ya Kwanza Mkupuo wa Kwanza hapo katika hospitali ya Makao Makuu Saateni.

Hata hivyo Kanali Jabir amewataka wahitimu hao kutoridhika na mafunzo waliyoyapata na badala yake wajiendeleze kielimu ili kuweza kutoa huduma nzuri zaidi katika hospitali mbali mbali za JKU.

Nae Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Luteni Kanali Saidi Omar Said amesema kuwa jumla ya wanafunzi ishirini wamehitimu mafunzo yao ya huduma ya kwanza kwa muda wa mwaka mmoja na mwezi mmoja katika masomo ya nadharia na vitendo ambayo yatasaidia kupunguza upungufu wa wahudumu wa afya katika hospitali za JKU.

Akisoma Risala kwa niaba ya wahitimu wenzake Praiveti Nadhra Ramadhan Iddi amesema kuwa licha ya mafanikio waliyoyapata lakini pia kuna changamoto kama vile upungufu wa vifaa vya kufundishia,ukosefu wa darasa maalumu pamoja na ukosefu wa posho la walimu.

 

Skuli ya Ufundi JKU Mtoni yafanya Uchaguzi.

Soko la Munduli lamfurahisha Dkt. Mwinyi.


WASILIANA NASI
  • Email: info@jkuz.go.tz
  • P.O.Box: 985
  • Fax: 0242232149
  • Tel: 0242238030
WALIOTEMBELEA TOVUTI