Email: info@jkuz.go.tz  |  P.o.Box: 985  |  Tel: 0242238030  |  Fax: 0242232149


Logo
HABARI NA MATUKI0

MKATABA WA UJENZI WA VIWANDA VYA MAONYESHO NYAMANZI

Created at 4 months ago

Mkuu wa JKUZ

Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Ndugu Ali Khamis Juma amelitaka Jeshi la Kujenga Uchumi (JKU) kuanza Rasmi Ujenzi Viwanja vipya vya Maonesho vilivyopo Nyamanzi Wilaya ya Magharibi B Unguja.

          Ameyasema Hayo wakati wa Hafla fupi ya Kusaini Mikataba ya Ujenzi wa Viwanja vya Maonesho mbalimbali iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar uliopo kusini Mjini Zanzibar.

          Amesema Ujenzi Huo umetokana na  Agizo la Mh. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Doc.Hussein Ali Mwinyi la kuboresha viwanja mbalimbali ili kupisha eneo la Maisara kufanyika Shughuli nyengine za kimaendeleo.

          Kwa upande wake Mkuu wa Utawala wa JKU Kanali Haji Ali Ali amesema JKU itahakikisha inajenga Viwanja hivyo kwa Ubora na wakati uliopangwa ili kuunga mkono jitihada za Serekali katika kuwaletea Maendeleo Wananchi wake.

          Hivyo ameiomba Wizara hiyo kutowa mashirikiano katika kila hatua ili kuondosha changamoto zinazoweza kujitokeza wakati wa utekelezaji wa Mradi huo.

MKUTANO MKUU WA JKU WA MWAKA 2022-2023

WAHITIMU WA KOZI YA UONGOZI MDOGO INT 018/2023 JKU DUNGA KUONYESHA UKOMAVU WAO KATIAK MAFUNZO


WASILIANA NASI
  • Email: info@jkuz.go.tz
  • P.O.Box: 985
  • Fax: 0242232149
  • Tel: 0242238030
WALIOTEMBELEA TOVUTI