Email: info@jkuz.go.tz | P.o.Box: 985 | Tel: 0242238030 | Fax: 0242232149
Mganga Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Meja SO Said akimkaribisha Mkuu wa JKU katika Ukaguzi wa Hospitali ya Makao Makuu JKU Saateni Mjini Zanzibar
Kuazishwa kwa JKU kulienda sambamba na uazishwaji wa vituo vya afya. Hospitali ya kwanza ilianzishwa katika Makao Makuu ya JKU Vuga mwaka 1977. Mganga mkuu wa kwanza katika hospitali hiyo alikuwa Dkt. Ramadhan Moh’d Mandoba kutoka Wizara ya Afya. Mganga mkuu huyu alikuwa akisaidiana na Praveti Abdalla Moh’d Khamis na Praveti Neema Khamis Sheha kutoka JKU.
Mwaka 1982 Makao Makuu ya JKU ilipohamia Saateni hostpitali hiyo nayo ikahamishiwa Saateni. Ongezeko la vikosi lilienda pamoja na uanzishwaji wa vituo vya afya. Kufikia mwaka 2015 JKU ilikuwa na idadi ya vituo vya afya 10 Unguja na Pemba. Jeshi la Kujenga Uchumi hutoa huduma za afya kwa askari, watumishi wa umma, vijana wa kujitolea, familia pamoja na jamii kwa ujumla. Huduma za afya pia hutolewa kwa wananchi wanaoishi jirani na makambi ya JKU.
Mpango wa matibatu kwa wananchi wa maeneo jirani na makambi ya JKU unaratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar na Jeshi la Kujenga Uchumi, ili kudumisha uhusiano kati ya wananchi na JKU. Huduma ya afya ya mama na mtoto zinatolewa bure katika hospitali zote za JKU. Chanjo za kitaifa hufanyika kwa ufanisi mkubwa kupitia vituo vya afya vya JKU.
Upimaji wa maambukizi ya virusi vya UKIMWI (VVU) unafanyika katika vituo viwili vya afya vya JKU vilioko Makao Makuu ya JKU – Saateni na Afisi Kuu JKU Pemba kwa wanajeshi na wananchi wanaoishi jirani na Kambi hizo.
HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA HOSPITALI YA JKU NI:-
a)Huduma za maradhi Aina zote
b) Huduma za Mama na Watoto
c)Huduma za Meno na Kinywa
d)Huduma za Maabara
e)Huduma za Ulta Sound
MWENGE WA UHURU 2020/2023 KUWASILI ZANZIBAR NA KUPOKELEWA KWA SHANGWE KATIK VIWANJA VYA ABEID KARUME
INT 018/2023 KUMALIZA MAFUNZO YA UONGOZI MDOGO JKU DUNGA
VIJANA JKU WAFAIDIKA NA MAFUNZO YA UVUVI NA UBAHARIA, WAFANIKIWA KUTENGENEZA BOTI AINA YA FIBER