MAJUKUMU YA JESHI LA KUJENGA UCHUMI ZANZIBAR (JKUZ)
MAJUKUMU YA MSINGI( Objectives)
1. Malezi ya Vijana
Vijana kufundishwa moyo wa kupendana bila kujali tofauti za itikadi, dini, kabila na kipato.
Kupenda kazi za mikono.
Kuthamini na kuendeleza mila, desturi na kudumisha utamaduni wa Taifa.
Kuwa raia wema, wanaojiamini, wanaojituma, wenye uzalendo na kuipenda nchi yao.
2. Ulinzi wa Taifa
Kuwapa vijana mbinu za kijeshi wawe Jeshi la akiba, kuwaandaa vijana watakaofaa kujiunga na vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama.
Kuwaandaa vijana kusaidia katika majanga mbalimbali, mfano mafuriko, moto na ajali mbali mbali.
3. Uzalishaji Mali
Ili kuwafanya vijana wa Kizanzibari waepukane na kusumba kuwa kazi za ofisini ndio njia pekee na bora inayomuwezesha mtu kuishi, JKU linahusika na uzalishaji mali kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri katika sekta mbali mbali mara baada ya kumaliza mkataba na JKU. Uzalishaji mali unaofanywa na JKU ni pamoja na:-
Kujenga na kukarabati majengo
Viwanda na Kilimo
Madini na Nishati
Utalii
Ulinzi kwa Taasisi binafsi na za kiserikali (JKU Security Guard Agency)
Maduka (Super Market)
Kuunganisha magari na mitambo
Huduma za elimu